Jumamosi , 17th Sep , 2022

Mwanasiasa Raila Odinga  aliyeshindwa kinyangányiro cha uchaguzi mkuu uliofanyika Kenya, ametaka tume ya uchaguzi ya mipaka ya nchi hiyo kufanyiwa marekebisho ili kuwa na matokeo sahihi ya chaguzi zijazo.

 Raila ambaye alishindwa kwa kura chache na Rais wa sasa  William Ruto , matokeo ambayo yalithibitishwa na mahakama ya juu ya nchi hiyo amesema kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika   9 August mwaka huu ulikua mbaya zaidi katika historia ya nchi hiyo.   

 

Akihutubia wabunge wa chama pinzani nchini humo, mwanasiasa huyo mkongwe amesema kuwa wabunge hao wana wajibu wa kuleta mabadiliko katika tume hiyo . Ameongea kuwa maamuzi ya mahakama kuu nchini humo ni pigo kwa demokrasia ya kenya.   

 Amesema kuwa kama muhimili wa mahakama hautabadiliswha , kuna hatari ya Kenya kutawaliwa na chama kimoja pekee.