"Rais Magufuli anatuunganisha" - Lema

Jumamosi , 12th Jan , 2019

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amedai kwamba baada ya watu kudharau katika haki kwa muda mrefu sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli anawaunganisha watanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli

Lema ametoa kauli hiyo ambapo ameiuliza maswali kuhusu biashara kufa, mahakama kutotenda haki pamoja na elimu na Afya ambako nako amesema hali ni mbaya.

Lema amedai kwamba Rais Magufli ni mpango wa Mungu na sasa kila mtu anaimba wimbo wa kufanana.

"Biashara zinakufa, Polisi/mahakama/DPP hawatendi haki?, elimu/afya ni mbaya?, matajiri mnaishi kama mashetani?, watumishi hamna amani?, wakulima hamna masoko?, Ndio. Rais Magufuli ni mpango wa Mungu. Tulidharau wajibu katika haki sasa anatuunganisha, tutaimba wimbo mmoja kabla ya uhuru kamili", amesema Lema.