Jumatatu , 20th Mei , 2019

Polisi waliomkamata mbunge wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine, wameshtakiwa katika Mahakama ya Kijeshi wakikabiliwa na mashtaka ya kutumia nguvu kupita kiasi.

Askari wakimkamata Bobi Wine

Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni amesema hakubaliani na nguvu ambayo Polisi wametumia kumkamata Bobi wine, kwani walitakiwa kutumia njia nyingine na si nguvu kama walizozitumia.

Maafisa wa polisi waliharibu gari la mbunge huyo wakati alipotiwa nguvuni, Aprili 22, 2019, ambapo sasa watakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya nidhamu ya polisi kwa matumizi ya nguvu kupita kiasi, kwa mujibu wa Msemaji wa polisi wa nchi.

Maafisa wa kikosi cha polisi cha kupambana na ghasia (FFU) walivunja madirisha ya gari la Mbunge huyo wa jimbo la Kyadondo Mashariki kwenye barabara ya Busabala alipokuwa akielekea kwenye eneo la 'One Love Beach' kufanya tamasha la muziki wake aliloliita 'Kyarenga Extra' ambalo baadae lilizuiwa na maafisa wa usalama.