Zitto ameyasema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara Mbagala Jijini Dar es salaam mkutano ambao uliandaliwa na chama cha Act Wazalendo kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.
''Wanafunzi ambao walisajiliwa katika programu maalumu ya kusaidia tatizo la upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi nchini katika Chuo Kikuu Cha Dodoma kati ya 7,802 wenye division 1V ambao walisajiliwa bila kuwa na vigezo ni 133 ni chini ya asilimia tatu ya wanafunzi wote'' amesema Zitto
''Rais wetu leo ambaye anajiita Rais wa maskini anawaita vilaza, bila kujali kwamba wazazi wa watoto hao maskini ndiyo walimpigia kura kutoka kila kona ya nchi hii ni vyema Rais akawa na akiba ya maneno''-amesema Zitto.
''Katika hali ya kawaida kiongozi mkuu wa nchi ndiyo yeye, yeye ndiye baba ni baba wa wenye akili na wasio na akili, ndani ya kundi lile kuna wanafunzi wenye division one mpaka divison three ambao walikuwa na uwezo wa kujiunga na kidato cha tano wakaamua kujiunga na programu hii maalumu ili kwenda kusaidia wadogo zao''-amesisitiza Zitto.


