
Uteuzi huo wa Mh. Biteko umefanyika leo Januari 6 na unaifanya Wizara ya Madini kuwa na Waziri ambaye ni Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wawili akiwemo Mh. Stanslaus Nyongo.
Wizara ya Madini ilitengwa kutoka kwenye Wizara ya Nishati na Madini na kuwa Wizara inayojitegemea kutokana na upana wake.
Mh. Biteko pia alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyoteuliwa na Rais Magufuli ndani ya mwaka 2017 kuchunguza madini ya Tanzanite.