Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Rais Magufuli aomba neno Vyama vya Upinzani

Jumatatu , 9th Dec , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, katika hotuba yake leo mkoani Mwanza, ametoa fursa kwa viongozi mbalimbali pamoja na wa Vyama vya Upinzani, akiwemo Freeman Mbowe na Profesa Ibrahim Lipumba, kutoa salamu kwa wakazi wa Mkoa huo.

M/Kiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Akizungumza leo Desemba 9, 2019, katika Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania, Mbunge wa Hai Freeman Mbowe wakati akitoa salamu zake kwa wananchi, amemuomba Rais Magufuli, kutumia siku hiyo kuleta maridhiano yenye mshikamano na upendo, yatakayoleta amani na Demokrasia kwa Taifa.

"Ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango, tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu Demokrasia, tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano na Mh Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa, kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia, kaliweke Taifa katika nafasi ya utengamano" amesema Mbowe.

Kwa upande wake Profesa Lipumba amesema kuwa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, lipo jukumu la kuhakikisha Demokrasia inakuwepo.

"Natoa pongezi kwa Watanzania wote, kwa kusherehekea miaka 58 ya Uhuru, mimi nilikua naingia darasa la nne, nampongeza Rais kwa kazi aliyoifanya, namuomba ajue anajukumu la kujenga demokrasia kwenye nchi yetu kuelekea Uchaguzi 2020" amesema Profesa Lipumba.

 

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali