Jumamosi , 12th Jan , 2019

Wafanyakazi Mkoani Irtinga wamelazimika kufanya maandamano maalum ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli juu ya maamuzi yake uamuzi wake kurudisha matumizi ya kanuni za kikokotoo cha zamani.

Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Hivi karibuni Rais Magufuli aliagiza kuanza kutumika tena kwa kanuni za zamani kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kufuatia kuibuka kwa sintofahamu, kwa wafanyakazi wa sekta mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati akipokea maandamano hayo Mkuu wa Mkoa Iringa, Ally Hapi amesema, "zawadi pekee ya kumpa Rais Dkt John Pombe Magufuli, ni kuendelea kutoa ushirikiano kwake kwa kumpongeza kwa kazi nzuri, na mimi Mkuu wenu wa Mkoa nasema sitasafiri kwenda nje nitakaa hapa hapa kufanya kazi".

"Nataka kutoa agizo kwa watendaji wote serikalini marufuku kunyanyasa wafanyakazi ama kumtoa mfanyakazi kwa hila, hataondolewa mtumishi popote bila mimi mkuu wa mkoa kujiridhisha, pia sitakubali kuona dokezo la mtu linakaliwa ili kuomba rushwa" ameongeza Hapi

Katika maandamano hayo pia wakuu mbalimbali wa wilaya akiwemo wa Iringa Mjini, Richard Kasesela pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdallah nao walishiriki ili kumpongeza Rais Magufuli.