Rais Magufuli amtumbua balozi

Alhamisi , 8th Nov , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi na kumrejesha nchini aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, Alphayo Kidata.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Novemba 8, na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe imesema kuwa utenguzi huo ulianza Novemba 5, 2018 pia ameondolewa hadhi ya Ubalozi.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametengua uteuzi wa balozi wa Tanzania nchini Canada Bw. Alphayo Japani Kidata na kumuondolea hadhi ya ubalozi", amesema Dkt. Mnyepe.

Bwana Alphayo Kidata.

Kabla ya kuteuliwa kuwa balozi wa Canada Kidata alikuwa Katibu Mkuu, Ikulu  ambaye aliteuliwa Machi 25, 2017 akitokea Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo alikuwa Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo.