Jumatano , 9th Feb , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba mtangulizi wake Hayati Dkt. John Magufuli, alimuachia urithi mzito katika masuala ya miundombinu na kuahidi mawazo yote aliyoyaanzisha atayatekeleza kikamilifu.

Kushoto ni Rais Samia Suluhu Hassan, na kulia ni Hayati Dkt. John Magufuli

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 9, 2022, wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya wa nje wa jiji la Dodoma.

"Siku kama ya leo mimi mwenzenu toka asubuhi huwa nasikia sauti ya mtangulizi wangu Hayati Dkt. John Magufuli, ananiambia kuhusu miradi hii, kuhusu Dodoma kuwa Makao Makuu, kuhusu mambo mengi," amesema Rais Samia

Tazama video hapa chini