Jumatano , 6th Oct , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewataka wanaume ambao wametelekeza watoto wao na kuacha kuwahudumia kwa sasa wasijifiche wanachopaswa ni kuwajibika kwa kushirikiana na wazazi wenzao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 6, 2021, jijini Dodoma, mara baada ya kumpongeza Mtendaji Mkuu wa Mahakama kwa kutenga chumba maalum cha kunyonyeshea ndani ya jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki pamoja na kuanzisha vituo jumuishi mahususi vya kushughulikia masuala ya kifamilia, mirathi, talaka, ndoa, malezi na matunzo.

Tazama video