Jumamosi , 10th Sep , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewataka wazazi na walezi nchini kuwaruhusu watoto wao kushiriki kwenye Mabaraza ya watoto yaliyopo katika ngazi za Kata hadi Taifa kwani katika mabaraza hayo ndipo vipaji vya watoto hao vinajengwa

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa na mtoto Victor

Akitoa Salamu  za Rais Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, wakati wa kumkabidhi bendera ya Taifa mtoto Victor Paschal Tantau, anayetarajiwa kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Watoto Duniani utakaofanyika nchini Denmark kuanzia tarehe 13 hadi 16 Septemba, 2022.

Amesema kuwa Watoto wanastahili haki ya kushiriki na kushirikishwa kwenye masuala yanayowahusu. ikiwa ni kutekeleza Haki hiyo ya Msingi kwao na inayotambuliwa na Baraza la Usalama la Umoja la Umoja wa Mataifa likihusisha viongozi wa nchi wanachama wa Umoja huo kwenye mkutano maalum iliofanyika tarehe 8 hadi 10 Mei, 2002 ikiwa na maazimio  kadhaa likiwemo azimio la kuunda chombo maalum kwa ajili ya ushiriki na ushirikishwaji wa Watoto katika masuala yanayowahusu.