Jumatatu , 12th Sep , 2022

Tanzania imesema zoezi la sensa na makazi limefanikiwa kwa hatua mbili za mwanzo, huku hatua ya tatu ya kuchakata na kuchapisha taarifa ikiwa inaendelea ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akitarajiwa kutangaza matokeo ya zoezi hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Akizungumza hii leo Septemba 12, 2022, walipotembelewa na Balozi wa China nchini Tanzania, Kamisaa wa Sensa Tanzania visiwani, Balozi  Mohamed Haji Hamza, amesema zoezi hilo limekamilika kwa hatua mbili ikiwemo maandalizi ya zoezi lenyewe huku kwa sasa likiwa katika hatua ya tatu ambayo ni baada ya zoezi la sensa ambapo wameanza kuchakata na kuchapisha taarifa za matokeo ya zoezi la sensa lililo kamilika hivi karibuni.

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania chen Mingijan, ameipongeza Tanzania kwa kufanikisha zoezi hilo na kusisitiza China itaendelea kuisaidia Tanzania katika kuimarisha masuala ya ya takwimu kwa mustakabali wa maendeleo ya mataifa hayo mawili.

Naye Mtakwimu Mkuu wa serikali Dokta Albina Chuwa, amesema ujio wa Balozi wa China NBS ni kutokana na makubaliano walioingia ambayo yatadumu kwa miaka mitano  huku nchi hizo mbili zikitarajiwa kubadilishana takwimu za matokeo ya sensa ili kusaidia katika maendeleo.