
Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 10, 2021, Ikulu ya Dar es Salaam, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao, ikiwa ni ziara rasmi ya kiserikali ya Rais Kenyatta.
"Nimemuambia kwenye mbuga zangu kule Ngorongoro na Serengeti, kuna madume mawili tu ya Faru hayana wake, nikamuambia sio vibaya hawa Faru wakioa Kenya, sisi tuko tayari kutoa mahari, tupate Faru jike kutoka Kenya yaolewe Tanzania, mdogo wangu amenikubalia siku ya kuwapokea tukate keki ya hiyo ndoa," amesema Rais Samia