
Rais wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Mugabe
Familia ya rais huyo wa zamani imeiambia BBC kuwa amefariki akipigania afya yake, ambapo alikuwa akiugua kwa muda mrefu.
Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa amemzungumzia mzee Mugabe katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa ni kiongozi shupavu na aliyeongoza vita ya kupinga ukoloni pamoja na kuwapigania watu wake.
Cde Mugabe was an icon of liberation, a pan-Africanist who dedicated his life to the emancipation and empowerment of his people. His contribution to the history of our nation and continent will never be forgotten. May his soul rest in eternal peace (2/2)
— President of Zimbabwe (@edmnangagwa) September 6, 2019
Robert Mugabe alizaliwa Februari 21, 1924 katika nchi iliyojulikana kama Rhodesia ambayo sasa ni taifa la Zimbabwe.
Katika historia yake ya mapambano ya kuipigania nchi hiyo, Mugabe aliwahi kufungwa jela kwa zaidi ya miaka 10 baada ya kuikosoa serikali ya kikoloni ya Rhodesia mwaka 1964.
Baada ya kuiongoza Zimbabwe kwa miongo mitatu, aliondolewa madarakani kwa nguvu ya jeshi mwishoni mwa mwaka 2017.
FAMILIA
Mugabe ana watoto watatu na mke wake wa pili ambaye ni Grace Marufu na walifunga ndoa mwaka 1996. Mwaka mmoja baadaye wakafanikiwa kupata mtoto wa tatu, kipindi ambacho Mugabe alikuwa na miaka 73.
ELIMU
Mugabe ana shahada 7, alipata digrii yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Fort Hare, Afrika Kusini. Akiwa gerezani pia aliweza kusoma na kupata shahada zingine kwenye Usimamizi, Sheria, Elimu na Sayansi.
Rais Magufuli naye ametoa pole zake.
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu na Baba wa Taifa la Zimbabwe Mzee Robert Mugabe. Afrika imepoteza mmoja wa viongozi Jasiri, Shupavu, Mwanamajumui wa Afrika na aliyekataa ukoloni kwa vitendo. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.
— Dr John Magufuli (@MagufuliJP) September 6, 2019