Jumatatu , 3rd Oct , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewataka Mawaziri kuhakikisha wanaijua mipaka yao na kwamba wasiivuke bila maelekezo kutoka juu.

Mawaziri walioapishwa leo (Kushoto ni waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Stergomena Tax, katikati ni Waziri wa Ulinzi Innocent Bashungwa na wa mwisho kulia ni Waziri wa TAMISEMI Angellah Kairuki)

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 3, 2022, Ikulu ya jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuwaapisha Mawaziri aliowateua hapo jana, ambaye ni Waziri wa Ulinzi Innocent Bashungwa, Waziri wa TAMISEMI Angellah Kairuki na Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Stergomena Tax.

"La pili ni kujua mipaka, mipaka ya kwamba nchi hii ina mamlaka na mamlaka uliyowekewa ina ukomo wake, unapotaka kuvuka lazima upata ruhusa ya mamlaka ya juu, sasa kujua mipaka yenu mpanapofanya kazi, kwenda juu pia kushuka chini," amesema Rais Samia