Ijumaa , 25th Dec , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, leo ameshiriki misa takatifu ya Sikukuu ya Christmas iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Chamwino Ikulu mkoani Dodoma leo Desemba 25, 2020.

Rais Dkt. John Magufuli, akipitisha kapu la sadaka kwa waumini wakati wa ibada Takatifu ya Sikukuu ya Christmas

Katika ibada hiyo Rais Dkt. Magufuli pia amepitisha kapu la sadaka kwa waumini wa kanisa hilo.

Sikukuu ya Christmas huazimishwa kila ifikapo Desemba 25, kila mwaka, na wakristo husherehekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.