Jumanne , 24th Aug , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, tayari amekwishawasili nchini Zambia kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Mpya wa 7 wa Zambia Hakainde Hichilema.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, alivyowasili nchini Zambia hii leo

Tume ya Uchaguzi nchini Zambia Agosti 16, 2021, ilimtangaza Hakainde Hichilema, kuwa mshindi wa Kiti cha Urais katika uchaguzi uliofanyika Agosti 12 na kumshinda aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Edgar Lungu.

Mh. Hakainde Hichilema, anaapisha leo Agosti 24, 2021.