
Mkuu wa mkoa wa Songwe Omary Mgumba amesema kuwa kuwa gari hilo lilikuwa ofisini ndipo dereva wa gari hilo alipodanganya ofisini kuwa ana dharura na akaruhusiwa kutoka na gari ndipo akaenda kufanyia shughuli hizo
Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Songwe amesema kuwa wataendelea kuwashikilia na kuwakamata wamiliki wote wa magari hayo na hawatayatoa hadi pale watakapowaleta madereva wote waliokua wanaendesha magari hayo
Aidha Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Songwe ametoa wito kwa Wafanyabiashara, kufuata sheria za forodha ili kuepuka kukamatwa na magendo na sheria kuchukua mkondo wake