Ijumaa , 23rd Jul , 2021

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, ameonesha kukasirishwa na utaratibu usiofaa wa ukamataji wa magari kwenye maegesho yasiyo rasmi 'wrong parking' ambapo ameelekeza kuitishwa kikao cha pamoja baina yake, Wakurugenzi wa Halmashauri na TARURA ili kupatia ufumbuzi jambo hilo.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla

RC Makalla amefikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko mengi ya wananchi juu ya utaratibu mbovu unaotumika na kusema kama kiongozi kamwe hawezi kuruhusu jambo hilo liendelee.

Aidha, RC Makalla amesema amebaini pia baadhi ya vijana wanaofanya kazi hiyo wamekosa weledi na busara na wengi wao wamekuwa wakivizia mtu afanye kosa ili wamuadhibu badala ya kutoa elimu ili makosa yasifanyike.