Alhamisi , 15th Dec , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ameiagiza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, kufunga vifaa vya mashine ya mionzi ya CT - Scan  ambavyo tayari serikali imevinunua ili  wagonjwa waanze kupata huduma mbalimbali za uchunguzi wa kitababu

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametoa maagizo hayo wakati anafanya ziara  ya kukagua miradi   mbalimbali ya ujenzi  inayotekelezwa  katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya

Aidha RC Homera amepongeza uongozi mpya wa hospitali hiyo kujitahidi kuongeza ukusanyaji wa mapato