Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema bado mkoa huo unafursa ya kuongeza pato licha ya kutokuwepo kwa rasilimali Kama madini na vinginevyo Kama mikoa mingine.
''Bado mkoa una fursa ya kuongeza pato, Mkoa na Serikali tarehe 10 tutakua na mkutano na wenye viwanda na wafanyabishara lengo ni kutoa mrejesho wa Serikali imefanya nini maeneo yenye changamoto na ambayo bado, yako kwenye hatua gani''amesema RC Kunenge
Aidha ameongeza kuwa wanaamini kwa kufanya hivo kutaongeza ajira kwa wananchi na kudai kuwa huduma zinazozalishwa zitasaidia kutatua mahitaji mbalimbali katika jamii.