Ijumaa , 23rd Jul , 2021

East Africa Television imefanikiwa kufika nyumbani kwa marehemu Anna Mghwira mkoani Arusha na kuzungumza na majirani pamoja na mtoto wa pekee wa marehemu ambaye hata hivyo alisema bado ratiba ya mazishi haijapangwa.

Nyumbani kwa marehemu Anna Mghwira

Mama Anna Elisha Mghwira, amefariki dunia Julai 22, 2021, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha.
 
Marehemu Anna Mghwira aliwahi kuwa mgombea urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na baadaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
 

Tazama Video hapo chini