
Mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Rostam Aziz ametoa kauli hiyo alipokuwa Ikulu Jijini Dar es salaam alipofika ofisini hapo kwa kwa ajili ya kuzungumza mambo mbalimbali
hususani masuala ya kibiashara.
Akizungumza mbele ya Rais Magufuli Rostam Aziz amesema, "nimekuja kumuona Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi, na kumtakia heri juu ya kazi kubwa anayoifanya na kama mfanyabiashara kinachofanyika hivi sasa ni kutengeneza misingi ya uchumi."
"Anachokifanya sasa hivi Rais Magufuli kiuchumi tunasema anaondoa uchafu, ili pawe na uwanja sawa watu waweze kufanyabiashara zao na hivyo uchumi utaweza kukua," ameongeza Rostam Aziz.
Itakumbukwa kuwa mapema mwezi huu Jeshi la polisi nchini liliripoti kumshikiria moja ya ndugu wa mfanyabishara huyo Ikram Aziz na kumfikisha mahakamani, kwa makosa ya kukutwa na nyara za serikali bila ya kuwa na kibali.
Aidha wakati huohuo Rais Magufuli amekutana na viongozi mbalimbali wa vyama vya kisiasa akiwemo Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR Mageuzi James Mbatia na Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo.