Jumatano , 8th Apr , 2020

Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi ametoa Shilingi Bilioni 1 na kwa ajili ya kununulia vitakasa mikono ambavyo vitatumiwa na wasafiri wa daladala kwa Jiji la Dar es Salaam na Zanzibar ili waweze kutumia kabla ya kupanda usafiri huo ikiwa ni hatua za kujikinga na Virusi vya Corona.

Mfanyabiashara Rostam Azizi.

Hayo ameyabainisha leo Aprili 8, 2020, Jijini Dodoma, ambapo yeye pamoja na wadau mbalimbali, wametoa msaada kwa Serikali wenye thamani ya Shilingi Bilioni 6.226, kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona, uliopokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Aidha Rostam amempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kuwaongoza Watanzania kwa hekima na busara na kuwaepusha na taharuki kama ilivyotokea katika Mataifa mengine, ambapo pia amempongeza Waziri Mkuu na Waziri wa Afya kwa namna ambavyo wanavyoshiriki katika kukabiliana na Virusi vya Corona.