Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Royal Tour haitakuwa na maana tusipolinda vivutio

Jumamosi , 14th Mei , 2022

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mkomi amewataka Maafisa na Askari wa Uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi kuhakikisha wanalinda vivutio vya utalii vilivyopo nchini

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mkomi akizungumza na Maafisa na Askari wa Uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi ambapo amewataka kuhakikisha wanalinda vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuleta maana ya uwepo wa Filamu maarufu ya ‘The Royal Tour’

Amesema kuwa kuwa Filamu maarufu ya ‘The Royal Tour’ iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan haitakuwa na maana kama vivutio hivyo havitalindwa

Naibu Katibu Mkomi  ameyasema hayo Ijumaa Mei 13, 2022 alipokuwa akifunga mafunzo ya kijeshi kwa Maafisa na  Askari 190 kutoka TFS, TANAPA, NCAA na TAWA katika kambi ya mafunzo ya kijeshi Mlele mkoani Katavi.
" Filamu ile imezinduliwa  kwa lengo la kuhamasisha shughuli za utalii na Uwekezaji nchini na tangu izinduliwe kila Mtanzania na Dunia wanafahamu  Tanzania kuna nini" amesema Naibu Katibu mkuu huyo.

Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo, tangu filamu hiyo izunduliwe inafanya vizuri Kimataifa na tayari Marekani  imeoneshwa katika vituo 300 kati ya vituo 355 vilivyoripotiwa kuonesha filamu hiyo.

Amesema mafunzo hayo yakawe chachu ya kuimarisha sekta ya utalii na  kuhakikisha Watalii wanapata huduma katika mazingira bora ili kuendana na maono ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Amewaeleza  Wahitimu hao kuwa  wana wajibu wa kulinda misitu, wanyamapori, malikale na vyote ambavyo vinawavutia watalii kuja kutembelea.

" Niwaombe Wahitimu mkatanguliza mbele uzalendo kwa kuhifadhi na kulinda vivutio vyote vya utalii vitakavyokuwa chini yenu, msipotoa huduma nzuri kwa watalii Filamu ya Royal Tour haitakuwa na maana yoyote" amesisitiza Naibu Katibu Mkuu.

Kwa upande wake Mratibu wa Jeshi la Uhifadhi, Fidelis Kapalata amesema mafunzo hayo waliyoyapata katika yanakwenda kubadili mfumo wao kufanya kazi hususan katika kipindi hiki ambacho ujio wa watalii utakuwa mkubwa kufuatia kuzinduliwa kwa Filamu maarufu ya Royal Tour

Mwakilishi wa Kamishna wa Uhifadhi – TFS, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia – Utawala (SACC-Admn), Luoga Erasto anasema ni matarajio ya Jeshi la Uhifadhi – TFS baada ya mafunzo hayo wahitimu watakwenda kuishi utamaduni wa kijeshi na kuongeza kasi, ufanisi na uzalendo katika utekelezaji wa majukumu ya uhifadhi wa rasilimali za nchi.

“Niipongeze Wizaya ya Maliasili na Utalii kwa kuratibu mafunzo haya yenye lengo la kubadirisha mfumo wa utendaji toka ule wa kiraia na kuwa wakijeshi, sasa taasisi zote za Wizara zinakuwa na mfumo mmoja wa kijeshi ambao utasaidia katika mabadiliko ya kiutendaji,” anasema SACC Luoga.

Katika mahafali hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Filberto Sanga aliomba Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia uwezekano wa kuwapangia kazi wilani mwake baadhi ya wahitimu kutoka kila taasisi ya uhifadhi ili waweze kulinda maliasili zilizopo mkoani Katavi kwa kile alichodai mkoa huo umebarikiwa vivutio vingi vya utalii na vingi vikiwa wilayani Mlele.

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali