Moto uliokuwa ukiteketeza baadhi ya matanki ya mafuta ya Lake Oil.
Akizungumza na EATV &EA Radio Digital, leo Januari 9, 2020, Kamanda Kakwale amesema licha ya kufanikiwa kuuzima moto huo, Askari mmoja wa Jeshi la Zimamoto alipata mshituko baada ya kuingia kwenye chemba ambayo moto ulikoanzia na kuuzima.
"Mota ilipata hitilafu za kiufundi ambayo ilizalisha cheche za moto kutoka kwenye chemba ndogo ya chini, madhara yaliyotokea ni mwenzetu wa uokoaji mmoja, moshi ulimuingia kwenye kinywa na kupata mshituko kidogo" amesema Kamanda Kakwale.
Aidha Kamanda Kakwale ameongeza kuwa hadi sasa bado uongozi wa kampuni ya mafuta ya Lake Oil, haijawapelekea ripoti kamili inayoonesha ni athari kiasi gani imetokea.

