Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

RPC Kilimanjaro adai tuhuma za Sabaya si za kweli

Ijumaa , 24th Jan , 2020

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limesema, hakuna hujuma wala uharibufu wa miundo mbinu ya Reli katika eneo la Kijiji cha Rundugai wilaya ya Hai, kama ilivyoelezwa na Mkuu wa wilaya hiyo ,Lengai Ole Sabaya.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na RPC Kilimanjaro Salum Hamdun.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Salum Hamdun, amesema kuwa baada ya DC kutoa tuhuma hizo na kuagiza wafanyabiashara wawili wa Mabasi ya Abiria, kujisalimisha polisi, walitii agizo hilo na baada ya kutoa maelezo walitoka kwa dhamana.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa hakuna miundombinu ya Reli iliyoharibiwa au kuhujumiwa katika himaya hii kwa maana ya kipande cha kutoka Moshi kuelekea Arusha, ambapo mpaka sasa kimeshakarabatiwa kwa Kilomita 23 na kazi inaendelea" amesema RPC Kilimanjaro.

January 19, 2020, Mkuu wa wilaya ya Hai  Lengai Ole Sabaya, akiwa katika kijiji cha Rundugai akikagua ukarabati wa Reli, alitoa agizo kwa wafanyabiashara wawili wa mabasi ya Lim Safari na Machame Safari ambao ni Rodrick Uronu na Clemence Mbowe, kujisalimisha katika kituo cha Polisi cha Bomang'ombe kwa tuhuma za kuunda genge la uhalifu ili kuathiri usafiri wa Treni ya abiria kati ya Dar es Salaam ,Moshi na Arusha.
 

HABARI ZAIDI

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP

Mbunge wa Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi

"Ndege ijayo ipewe jina la Mwl Nyerere" - Profesa

Baadhi ya Wanachi wa Kata ya Msowero, wakiwa Katika Mkutano wa Hadhara na Mkuu wa Wilaya

Mwenyekiti atiwa mbaroni kwa kuuza mlima, Msowero

Sehemu iliyokumbwa na Mafuriko Kusini mwa Brazil

Wanaokufa kutokana na mafuriko waongezeka Brazil

Baadhi ya Wabunge Wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi

Serikali yashauriwa kuwa bunifu sekta ya usafiri