
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto (kulia) na kushoto ni Freeman Mbowe akiwa amelazwa wodini
Muroto amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma, kutoa taarifa juu ya shambulio ambalo amefanyiwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freema Mbowe.
''Onyo kali kwa wanasiasa na mtu yeyote atakayetumia tukio hili kwa namna yoyote ile ikiwemo kujiongezea umaarufu au kuingilia uchunguzi wa polisi, tutamshughulikia kweli'', amesema.
Aidha amethibitisha kweli kushambuliwa kwa Freeman Mbowe na amesema wanaendelea na uchunguzi ikiwemo kuwahoji majirani na watu wengine huku akisisitiza kuwa hataachwa mtu yeyote ambaye anahusika.
Zaidi tazama Video hapo chini