
Washtakiwa wa kesi ya kughushi nyaraka na kijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha dola milioni 550 za marekani kwa serikali kutoka Bank ya Standard ya Uingereza Dkt. Harry Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomon wameshinda rufaa waliyokatiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka DPP, katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.
Mahakama imetoa nafasi kwa upande wa Jamuhuri kufanya marekebisho ya mashtaka kwa kosa namba 8 la kutakatisha fedha ambalo rufaa yake imegonga mwamba na kushauri kama wakiona inafaa waweze kurekebisha shtaka zima la kesi hiyo.
Katika hoja za pingamizi wakili Alex Mgongolwa kwa niaba ya mawakili wenzake Dk. Ringo na Majura Magafu amesema uamuzi wa mahakama ya kisutu kufuatia shtaka hilo hauwezi kukatiwa rufaa kwa kuwa si uamuzi ambao umemaliza au umehitimisha kesi hiyo.
Washtakiwa hao bado wana makosa 7 ya kujibu dhidi ya shitaka hilo.
Kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 18, mwezi wa 5 katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.