
Waziri mkuu wa Tanzania, Mizengo Kayanza Peter Pinda akisalimiana na wanafunzi wa shule ya awali hivi karibuni.
Mhe. Pinda ametoa agizo hilo wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa Rukwa mara baada ya kupokea taarifa ya Mkoa huo, Ikulu ndogo, mjini Sumbawanga.
Waziri Mkuu aliwasili mkoani Rukwa akitokea Dodoma ambapo amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye ibada ya kumuweka wakfu Askofu Mteule, Conrad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa katika Uwanja wa Nelson Mandela, Mjini Sumbawanga.
Akifafanua kuhusu tatizo la madawati, Waziri Mkuu alisema ni lazima wajipange kama mkoa ili waweze kusaidia juhudi za Serikali kupunguza tatizo la madawati kwa watoto wetu wa shule za msingi nchini.