Ijumaa , 16th Sep , 2022

Wakala wa usambazaji maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA Wilaya ya Morogoro imeagizwa kuhakikisha inawasimamia kikamilifu wakandarasi wanaotekeleza miradi nane ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 30 wilayani hapo ili ikamilike kwa wakati.

Hilary Sagara, Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro

Maagizo hayo yametolewa baada ya kamati ya usalama ya wilaya ya morogoro ikiongozwa na Kaimu Katibu Tawala Bw, Hilary Sagara kufanya ziara ya siku tatu ya kukagua miradi nane ya maji huku akisisitiza wananchi wanahitaji sana miradi hiyo, ili waweze kuwa uhakika wa upatikanaji wa maji safi na salama.

Aidha ametaka hatua za kisheria kuchukuliwa kwa baadhi ya wakandarasi wambao wamekuwa wakitekeleza miradi hiyo tofauti na makubaliano.

Kwa upande wake  Kaimu Meneja wa RUWASA Shack Kimbwereza amebainisha faida za miradi hiyo kwa maeneo yanayotarajiwa kunufaika, ambapo watu zaidi ya kali moja wanatarajiwa kunufaika na miradi hiyo.

Awali wakizungumzia hali ya upatikanaji wa maji safi na salama kwenye maeneo yao, wananchi katika baadhi ya maeneo ya wilaya ya morogoro wameeleza hali ilivyo katika kwenye maeneo yao ambapo wamekuwa wakilazimika kutumia maji yasiyo salama kutoka kwenye mto Ngerengere.