
Jeshi hilo limesema kuwa linafanya uchunguzi kwenye eneo hilo kuhusu shambulizi hilo. .
Mgongano baina ya nchi hizo mbili umeongezeka toka mwezi March, wakati vikosi vya waasi wa M23 ambavyo Congo inaishutumu Rwanda kwa kuviunga mkono, vilipowashambulia wanajeshi wawili wa Congo.
Hata hivyo Rwanda imekua ikikana madai kwamba inawasaidia waasi hao.
Kundi hilo la waasi limekua likiisumbua serikali ya Congo toka mwaka 2012 na mwaka 2013.
Familia nyingi zimekimbia makazi yao huko kaskazini mwa jimbo la Kivu, zikielekea kwenye mpaka wa Uganda majini Bunagana.
Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linaloshugulikia wakimbizi nchini Uganda, Joel Boutroue, amesema kuwa maelfu ya wakimbizi wamewaili nchin iUganda siku ya jana