
Tundu Lissu
Awali akizungumza mahakamani hapo Wakili wa upande wa uetezi Peter Kibatala amesema kuwa, Lissu hajafika mahakamani hapo kutokana na na siku ya jana kuchelewa kukamilisha mchakato wake wa kurejesha fomu kwa ajili ya kuteuliwa na Tume ili aweze kugombea Urais kwani alitarajia kukamilisha mchakato huo saa 6:00 mchana lakini alikaa hadi saa 2:00 usiku.
"Ilikuwa imepangwa akitoka NEC saa sita atakapomaliza, ajiandae kurudi ili kuhudhuria Mahakamani leo lakini bahati mbaya alikaa hadi saa mbili na nusu usiku hali iliyopelekea kuharibu taratibu za usafiri alizozipanga, hivyo naomba Mahakama iridhie kuhairisha shauri hili na kupanga tarehe nyingine ambayo tunaamini atakuwepo", amesema Wakili Kibatala.
Mara baada ya mawasilisho hayo upande wa Jamhuri uliowakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali Renatus Mkude na Wakili wa Serikali mwandamizi Wankyo Simon, haukua na mapingamizi na kutoa rai shauri hilo liahirishwe hadi tarehe nyingine.
Lissu anakabiliwa na mashtaka ya uchochezi anayodaiwa kuyatenda Julai 17, 2017, katika eneo la Ufipa Kinondoni Jijini Dar es Salaam, ambapo inadaiwa alitoa maneno ya kichochezi kwa kusema kuwa Serikali inaendeshwa kibaguzi, kifamilia, kikabila, kidini na kikand.