
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. George Kahangwa
Akizungumza katika Kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio Dkt.Kahangwa amesema kuwa kutoikujua kuhusiana na mpango kazi ndio chanzo chakuwa na watendaji wasiojua wana wajibu gani wa kutimiza kwa taifa matokeo yake hawana la kufanya zaidi kukaa maofisini.
“Suala la mpango kazi halipaswi kiongozi akumbushe ni utaratibu wa kawaida wa kila ofisi hawa wanaohitahji kukumbushwa kuwa na mpango kazi kwa kweli wanalikosea taifa na ndio maana watu wakati mwingine hawajuui wafanye nini” amesema Dkt. Kahangwa
“Mpango kazi ni jambo la kusisitiza sana kwani mambo ya mpango kazi yanaaibisha yakiwa yanazungumziwa katika ngazi za juu ilhali kuna viongozi ambao wapo wanaotakiwa wawakague wenzao wa chini kuhusiana namipango kazi yao” ameongeza Dkt. Kahangwa
Aidha Dkt.Kahngwa amesifu tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kuhusiana na kufundishwa histori ya kwetu ambapo amesema kufanya hivyo kutasaidia kizazi hadi kizazi kujua tunapotoka na jambo tunalolifanya leo msingi wake ni upi kuliko kuwafundisha vitu ambavyo haviwakumbushi uzalendo wala chimbuko lao.