Jumatatu , 30th Aug , 2021

Mwili wa Hamza Mohammed aliyefariki dunia katika tukio la majibizano ya risasi kati yake na Jeshi la Polisi amezikwa usiku wa kuamkia leo Agosti 31, 2021, majira ya saa 2:30 usiku katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Hamza

Kwa mujibu wa Msemaji wa familia ya , Abdulrahm Hassan, amesema kuwa awali mwili huo ulitarajiwa kuzikwa saa 7:00 mchana katika makaburi hayo, lakini  ulichelewa kwa sababu ya kazi ya kutoa risasi zilizokwama kwenye mwili wake.

Hamza alizua taharuki siku ya Agosti 25, 2021, baada ya kuwauwa kwa risasi Askari wanne akiwemo mmoja wa Kampuni ya Ulinzi binafsi ya SGA maeneo ya daraja la Selander karibu na zilipo ofisi za Ubalozi wa Ufaransa wilayani Kinondoni.