
Lengai Ole Sabaya
Watuhumiwa waliochiliwa huru ni Sylivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Asey huku mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo Lengai Ole Sabaya akibaki magereza kuendelea na shauri hilo.
Mkurugenzi Msaidizi wa kutenganisha upelelezi na mashtaka Marternus Marandu, amesema mnamo Agosti 3, 2022, washtakiwa hao wanne waliandika barua katika ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa serikali kuomba kukaaa meza ya makubaliano ili kuweza kulipa faini na fidia.