
Kushoto ni Mbobezi wa masuala ya siasa Majid Mjengwa, na kulia ni Rais samia Suluhu Hassan
Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 30, 2021, kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, wakati hii leo Chama cha Mapinduzi (CCM) kinafanyana mkutano wake maalum wa kumuidhinisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho.
"Rais Samia ni kweli anakikuta chama kimesafishwa kwenye makandokando ya mali za chama, lakini pia anakikuta chama kina makundi, unapokuwa una wajumbe zaidi ya 1000 wanakusanyika mahala ni ajabu kutokufikiri kama kuna watu pia wanafikiri kimakundi, hivyo anatakiwa kuyayafanya hayo makundi yajielekeze kwenye ujenzi wa chama na nchi ambayo anaiongozi", amesema Majid
Aidha Majid ameongeza kuwa "Mwenyekiti mwanamke tunaweza tukatumia aina hiyo ya kutambulisha lakini huyu anakwenda kuwa Mwenyekiti wa CCM, sasa jinsia hiyo ni kitu kingine kabisa lakini Samia Suluhu siyo Mwenyekiti mwanamke isipokuwa ni Mwenyekiti wa CCM anayekwenda kuthibitishwa leo".