
Sudan Kusini
Bernard Aritua, Afisa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia (WB), amesema kuwa kama Benki ya Dunia hawawezi kutoa ufadhili wa kujenga miundombinu hasa barabara kutokana na ukosefu wa Sera za Kifedha na Kanuni za Sekta ya Uchukuzi nchini Sudan Kusini.
Benki ya Dunia imesema kwamba Sudan inapaswa kufanyia marekebisho Sera zake zenye changamoto kwa Misaada ambazo ni kukosa uwazi wa matumizi ya fedha kwenye taasisi zake pamoja na sheria zisizotabirika.
Hatahivyo, utafiti mpya uliofanywa na Mamlaka ya Uratibu wa Usafirishaji na Usafiri wa Kaskazini (NCTTCA), umeonesha Barabara za Sudan Kusini ndiyo mbaya zaidi katika eneo la pembe ya Afrika Mashariki.