
Naibu Waziri wa Fedha na Mpingo Mhe. Ashantu Kijaji
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mpingo Mhe. Ashatu Kijaji wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo bungeni ambapo amesema kuwa lengo la serikali ni kushusha zaidi hadi kufikia digiti moja.
Mhe. Ashatu ameongeza kuwa baada ya kufikia asilimia 10 ya tozo la kodi hiyo serikali itakaa na wadau ikiwemo vyama vya wafanyakazi ili kutafuta ufumbuzi wa ni namna gani wanaweza kushusha zaidi kutokana na ukuaji wa uchumi siku hadi siku.
Katika hatua nyingine Mhe Ashatu amesema kuwa serikali imedhamiria kupandikisha kiwango cha pensheni kwa wazee wastaafu hadi kufikia shilingi laki mbili na nusu kadri ya uchumi utakavyoimarika na mikakati tayari imeshaanza kuandaliwa.