Jumatano , 26th Oct , 2022

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa kuwezesha upatikanaji wa wataalam, dawa, vitendanishi na vifaa tiba.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfano wa Mji Mpya wa Serikali ya Korea Kusini

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Oktoba 26, 2022 baada ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) na Serikali ya Jimbo la Chungcheongbuck nchini Korea kusini.

Aidha Majaliwa amemueleza Gavana huyo kuwa, kutokana na mpango wa Serikali wa kuendelea kuimarisha eneo la utoaji huduma za afya, Serikali ya Tanzania inawakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kujenga viwanda vya dawa na vifaa tiba ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa dawa na vifaa tiba.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametembelea kituo cha KBio Health ambacho kinajishughulisha na utengenezaji wa dawa za binadamu na vifaa tiba kilichopo katika mji wa Chungbuk, Korea Kusini pamoja na eneo jipya la mji wa Serikali, lililopo Sejong nchini Korea Kusini.