Ijumaa , 6th Dec , 2019

Serikali mkoani Kagera imeshauriwa kuweka utaratibu, utakaowezesha wanafunzi wote wa Shule za Msingi na Sekondari kupata uji au chakula shuleni, ili kupunguza tatizo la mimba linalotokana na baadhi yao kudanganywa kwa chipsi.

Chips

Wakizungumza wakati wa kikao cha wadau wa elimu cha kutathmini maendeleo ya sekta hiyo, baadhi ya washiriki wamesema kuwa ni vigumu kuwaepusha wanafunzi wa kike na vishawishi, wakati wanashinda njaa shuleni, huku baadhi yao wakitoka nyumbani bila hata kunywa chai.

Akijibu hoja hizo Mwenyekiti wa kikao hicho, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amezitaka Halmashauri zote kushirikikana na Serikali za Vijiji na wananchi, kuweka utaratibu wa kupata uji au chakula shuleni.

Awali akisoma taarifa za utekelezaji katika kikao hicho, Afisa Elimu wa Mkoa wa Kagera Juma Mhina, amesema kuwa mimba kwa wanafunzi zimepungua kutoka 201 mwaka 2018 hadi kufikia mimba 65 Novemba 2019a