Jumatatu , 25th Jul , 2022

Waziri wa maji mheshimiwa Jumaa Aweso amesema serikali imetenga bilioni 24 ili kujenga miradi mikubwa ya maji 49 kupitia ziwa Tanganyika mkoani Kigoma, ili kumaliza tatizo la ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo yote ya mkoa huo

Waziri Aweso amesema hayo katika kikao kazi cha tathimini maandalizi ya shughuli za manunuzi kwa mwaka wa fedha 2022 2023 na kusema serikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji mkoani Kigoma kupitia ziwa tanganyika.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amewataka watumishi wa idara za maji kuacha tabia ya kubambikizia wananchi bili za maji na kuwapa wakati mgumu wa kutumia maji.

Kwa upande wao baadhi ya wabunge wameeleza uwepo wa changamoto za maji katika majimbo yao na kwamba suala la kubambikiziwa bili lifanyiwe kazi ili kuwarahisishia huduma wananchi.