
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt. Leonard Akwilapo (kushoto) wakati akizindua ripoti ya HakiElimu inayoitwa ‘Elimu tunayoitaka’ kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt. Leonard Akwilapo wakati akizindua ripoti ya HakiElimu inayoitwa ‘Elimu tunayoitaka’ ambayo imeelezea kuwa sera ya Elimu iliyopo haiendani na mahitaji ya Elimu kwa kizazi cha leo.
Dkt. Akwilapo amesema kuwa Ongezeko la Wanafunzi liendane na Uwekezaji katika Elimu, na wameipokea ripoti hiyo kama changamoto kwa Serikali na watayafanyia kazi yale yote yaliyoshauriwa ikiwemo sera ya Elimu kutokidhi mahitaji.
“Ongezeko la Wanafunzi liendane na Uwekezaji katika Elimu, tunaipokea hii ripoti kama changamoto kwetu na tutayafanyia kazi yale yote yaliyoshauriwa ikiwemo sera ya Elimu kutokidhi mahitaji”, amesema Dkt. Akwilapo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu Dkt. John Kalage amesema kuwa Elimu inayotakiwa Tanzania kwa sasa ni ile inayokuza uwiano na umahiri wa karne ya 21.