
Mgogoro wa eneo hilo umedumu kwa zaidi ya miaka 30 kati ya Kanisa Katoliki jimbo la Kigoma na wamiliki wa shule hiyo
Hayo yajajiri kutokana na kufukuta kwa mgogoro baina ya wamiliki wa shule hiyo ya Jumuiya ya wazazi CCM dhidi ya Kanisa Katoliki kuhusu kuchelewa kwa utekelezaji wa agizo la aliyekuwa waziri wa Tamisemi Innocent Bashungwa aliyeamuru wamiliki wa shule kuvunja sehemu ya majengo ya madarasa na maabara ya shule hiyo agizo lililopaswa kutekelezwa kabla ya tarehe 13 septemba 2022,
Kwa sasa baadhi ya majengo kama vyoo yamevunjwa siku kadhaa na watu ambao hawajatambuliwa.
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Hanafi Msabaha akieleza juu ya Uamuzi wa Barua ya aliyekuwa waziri wa Tamisemi Innocent Bashungwa amesema Wamiliki wa shule wanapashwa kupisha katika eneo hilo kwa kuwa Kanisa Catoliki ndio wamiliki halali.
Aidha Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akatoa nafasi kwa viongoziwa pande hizo kueleza tofauti zao katika kutekeleza agizo hilo.
Hatua hiyo inamfanya mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye Kutoa kauli ya Serikali akirejea maelekezo ya barua ya waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ya Julai 252022 kuwataka Jumuiya ya Wazazi kupisha eneo hio Baada ya Wanafunzi wa kidato cha Pili na cha nne kumaliza mitihani yao.