Alhamisi , 27th Oct , 2022

Wakati serikali bado ikiwa katika harakati za kuokoa uhai wa bonde la Ihefu ambalo ndilo chanzo kikuu cha Maji yanayotiririka katika Mto Ruaha, tayari Shirika la hifadhi za Taifa TANAPA wamechimba Visima virefu vya maji kwa ajili ya mifugo ya wakazi wa vijiji jirani na hifadhi hiyo.

Baadhi ya wafugaji katika moja ya kijiji kilicho jirani na hifadhi ya Ruaha wamesema walikuwa wakilazimika kuingiza mifugo hifadhini kutokana na hali ya ukame iliyopo sasa, lakini kwa sasa maji yapo kijijini na safari za kwenda hifadhi zitakoma 

Kwa upande wake Afisa ujirani mwema kutoka TANAPA Priscous Mrosso amesema kwa sasa wamejipanga kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya namna hiyo katika maeneo ya Vijiji vingine vinavyo zunguka eneo la hifadhi