
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja
Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Daudi aliyetaka kujua lini serikali itajenga kituo cha askari wanyamapori wilayani Itilima na maeneo yanayozunguka Pori la Akiba Maswa.
Amesema kituo hicho kitakachohudumia zaidi ya vijiji tisa kitakuwa na askari wa jeshi la uhifadhi na askari wanyamapori wa vijiji (VGS) kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu katika vijiji vya Longalombogo, Nding’ho, Lung’wa, Nyantugutu, Mbogo, Shishani, Pijulu, Ng’walali na Mwamakili.