Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Serikali yaomba kurekebisha adhabu ya makahaba

Ijumaa , 14th Sep , 2018

Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masauni ameliomba Bunge kufanya marekebisho ya sheria ya  adhabu ya makosa ya biashara  makahaba ambapo aliitaja kama ni miongoni mwa changamoto zinazopelekea biashara ya ukahaba kuzidi kufanyika licha ya jitihada za serikali kuitokomeza.

Pichani wakina dada wakipandishwa gari la Polisi baada ya kukamatwa wakifanya biashara ya ukahaba.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Pwani Zainabu Matitu ambaye alihoji "kwanini Jeshi la Polisi linawakamata wauzaji wa biashara hiyo bila kuwakamata wanunuzi pamoja na wapangangishaji wa biashara ya madanguro, ambapo alipendekeza kubomolewa kwa eneo la uwanja wa fisi badala yake kujengwe miundombinu ya maendeleo ili wahusika wafanye biashara halali"?

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Masauni amesema “..kumekua na changamoto mbalimbali nadhani bunge hili ni wakati muafaka  wa kuzitafakari, moja ni changamoto ya sheria, ukiangalia kwenye kanuni ya adhabu namba 176  (E) sura ya 16 adhabu ni faini isiyozidi shilingi 500 au 1000.., hivyo kuna haja kuangalia na kutafakari ili kazi kubwa inayofanywa ya kuwakamata wahusika na biashara ya ukahaba iwe na tija…”

Aidha Massauni amesema kupitia Wizara ya mambo ya ndani itashirikisha wizara nyingine ikiwemo Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi, katiba na sheria pamoja na wizara afya ili kumaliza tatizo la biashara ya Ukahaba nchini.

“…Tumendaa mkakati wa kushirikisha taasisi nyingine za serikali kama vile wizara ya  Tamisemi, wizara ya katiba na sheria na pamoja na ustawi wa jamii ili kupunguza na kumaliza vitendo hivi ambavyo ni kinyume na utamaduni wetu.” amesema Masauni.

HABARI ZAIDI

Mbunge wa Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi

"Ndege ijayo ipewe jina la Mwl Nyerere" - Profesa

Baadhi ya Wanachi wa Kata ya Msowero, wakiwa Katika Mkutano wa Hadhara na Mkuu wa Wilaya

Mwenyekiti atiwa mbaroni kwa kuuza mlima, Msowero

Sehemu iliyokumbwa na Mafuriko Kusini mwa Brazil

Wanaokufa kutokana na mafuriko waongezeka Brazil

Baadhi ya Wabunge Wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi

Serikali yashauriwa kuwa bunifu sekta ya usafiri

Baadhi ya Wananchi Wakishudia Ajali Iliyomgonga Mwendesha Bodaboda

Watatu wanusurika kifo, scania ikimgonga bodaboda

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi (kulia) pamoja na Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk Kiva Mvungi (kushoto) wakimpatia vifaa kinga mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa madereva bodaboda wa jiji la Arusha.

Bodaboda 200 Jijini Arusha wanolewa na kufundwa