Alhamisi , 24th Nov , 2022

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, amesema kwamba mlango wa ndege iliyopata ajali Novemba 6, 2022, Bukoba mkoani Kagera ulifunguliwa na mhudumu wa ndege kwa kushirikiana na abiria.

Ndege ya Precision Air ilivyopata ajali

Taarifa hiyo imetolewa hii leo na Waziri Profesa Makame Mbarawa, wakati akitoa taarifa ya awali ya ajali ya ndege hiyo.

"Mlango wa ndege ulifunguliwa na mhudumu wa ndege kwa msaada wa abiria, hata hivyo wananchi waliokuwa wanafanya shughuli za uvuvi walifika eneo la ajali dakika tano baada ya ndege kuanguka," amesema Profesa Mbarawa.

Aidha akizungumzia taarifa rasmi ya ndege Profesa Mbarawa amesema, "Timu ya uchunguzi ya ajali ya ndege na matukio ya ndege itatoa maelezo ya awali ndani ya siku 14 baada ya ajali, ambayo itafuatiwa na ripoti ya awali itakayotolewa ndani ya siku 30 na ripoti kamili itatolewa ndani ya miezi 12 baada ya ajali kutokea,".

Ajali ya ndege ya Precision iligharimu maisha ya Watanzania 19.