
Choo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua matokeo ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria kwa mwaka 2015/ 2016.
Waziri Ummy amesikitishwa na ongezeko kubwa la ukuaji wa idadi ya watu, ongezeko la maambukizi ya malaria kwa watoto chini ya miaka 5 na ongezeko la mimba za utotoni nchini Tanzania.
Akiongelea idadi ya watu, Mhe. Ummy Mwalimu amesema, kila mwaka watoto milioni mbili huzaliwa ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 2.7 kila mwaka, Idadi ambayo amesema ikiendelea itapelekea huduma za Lishe, Elimu na Matibabu kutojitosheleza kutokana na ongezeko hilo.
Awali akitoa maelezo juu ya utafiti huo Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa matokeo ya utafiti huo yametoa mwelekeo mzima wa afya ya uzazi na mtoto hapa nchini, hivyo jamii kwa kushirikiana na serikali inatakiwa kuhakikisha watoto na akina mama wanaendelea kuwa na afya njema ili kutumikia taifa la Tanzania