Jumapili , 5th Jan , 2020

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, amesema wamevifutia usajili vyama vya ushirika 3436, baada ya kuonekana haviendeshwi kulingana na taratibu za ushirika na kukiuka taratibu zilizopo hivyo kuvifanya viwe vyama hewa.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga

Waziri Hasunga ameyasema hayo leo Januari 5, 2020, Jijini Dodoma, ambapo amemuagiza mrajisi wa vyama hivyo nchini, kuhakikisha anavifuta haraka iwezekanavyo, sambamba na kufanya uchunguzi ili kubaini madudu na hatua ichukue mkondo wake.

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga kwa mujibu wa sheria ya kilimo, ameidhinisha matumizi ya aina 40 za mbegu mpya za kilimo baada ya watafiti kujiridhisha na uwezo wa mbegu hizo, kwamba zinahimili hali ya hewa ya Tanzania hivyo zitaongeza upatikanaji wa chakula nchini na akiba ya mbegu.

Aidha Waziri Hasunga amesema Tanzania inapaswa kuzalisha tani laki 186,000 kwa msimu lakini bado kiwango hicho hakijafikiwa, hata nusu yake hivyo jitihada zaidi zinahitajika katika kuzalisha mbegu.